Header

Manchester United waitwanga Southampton 3-2 na kutwaa Ubingwa wa Kombe la EFL

Klabu ya Manchester United jana imetwaa Ubingwa wa Kombe la EFL baada ya kufanikiwa kuifunga Southampton Mabao 3-2 Magoli ya Manchesater United  yalifungwa na Jesse Lingard huku mabao mawili yakiwekwa wavuni na Zlatan Ibrahimovic na Mabao ya Southampton yakifungwa naManolo Gabbiadini.

Image result for man united 3-2 southampton efl winner

Wachezaji wa Man United wakishangilia Baada ya kukabidhiwa kombe la EFL

Southampton walionesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo lakini wakavunjwa moyo na uamuzi wa utata ulioipatia bao la ushindi Manchester United kunako Dakika za Mwisho za mchezo huo.

Oriel Romeu alipiga mwamba wa goli kabla ya Ibrahimovic kufunga kupitia krosi iliopigwa na Anders Herrea dakika tatu kabla ya mechi kukamilika na hivyobasi kuipatia ushindi Manchester United.

Na kwa ushindi huo umemfanya Kocha Jose Mourinho kutwaa taji la kwanza akiwa na Klabu hiyo ya Mashetani Wekundu.

Comments

comments

You may also like ...