Header

Haya ndiyo majibu ya Baraka The Prince baada ya kuulizwa nani mfalme wa Hip Hop Bongo?

Msanii Baraka The Prince ni moja kati ya wasanii ambao mara nyingi wanasikiliza muziki wa Hip Hop kwani karibia Interview nyingi kwenye Media huwa anaongea hilo sasa swali linakuja ni Rapa gani hapa Bongo yeye anamchukulia kama Mfalme wa Hip Hop? majibu yake bila ya kupapasa macho ni Lord Eyez.

Baraka The Prince amesema Lord Eyez ni msanii mkali sana kwenye Mashairi yake na ni moja ya wasanii ambao wanafanya kazi zinazodumu na hiyo ni sababu moja wapo ya kumsaini kwenye lebo yake.

“Ukiondoa mimi kufanya biashara na Lord Eyes mimi ni shabiki wake namba moja, nimesikiliza ngoma zake nyingi sana unaona ni ngoma kali sana sema jamaa alikosa usimamizi tu wa kazi zake, nimesikia kuna watu wana ‘diss’ Lord Eyes kusimamiwa kazi zake na mimi nachoweza kusema hao ni waoga wanajua Lord Eyes ana talent kubwa hivyo wameanza kumuogopa, mimi namuona Lord Eyes ni mfalme wa hip hop Bongo” alisema Baraka The Prince kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

Baraka kwa sasa anamiliki Lebo yake ya Muziki inaitwa ‘BANA’ na tayari ameshamsaini Lord Eyez.

Comments

comments

You may also like ...