Header

Sakata la Mama Ongea na Mwanao: Irene Uwoya awatolea uvivu Wema Sepetu na Batuli

Kukiwa bado kuna mvutano baina ya Wasanii wawili wakubwa kwenye kiwanda cha Movie nchini Wema Sepetu na Batuli baada ya wawili hao kukinzana kwenye kauli ya kulipwa na kutokulipwa na CCM kwenye Kampeni za uchaguzi mwaka 2015hasa hasa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao hatimae Irene Uwoya amewatolea uvivu wawili hao.

Madam Irene Uwoya amesema hawakustahili kulumbana na kuyaweka wazi mambo nyeti kama hayo ya malipo kwani ni dhahili kuwa walikuwa kimaslahi na si vinginevyo na huenda hata kwenye haya yanayoendelea wamelipwa kiasi fulani cha mtonyo.

Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa… Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia… Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamaniii… Kunavitu vingine ukiongea havina maana.” Ameandika Irene Uwoya kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuendelea kusema

Mfano mim ni CCM damu… Lakin kunavitu vinaboa sanaaa Kweli kada mzima wa CCM unasimama hazarani unasema tulilipwa kufanya campaign? hatakama lakini unafundisha Nin Jamiii? Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuyaamanisha nikwasababu tulilipwa? Unaiambia jamiii ulikuwa tayari kuwadanganya na mliwadanganya sababu mlilipwa? Hivi Kweli? Kwahiyo jamiii ione Chochote Tutachoonge wasikiamini maana yake tutakuwa tumelipwa? Kwahiyo ata mnayoyaongea mnataka kusema mmelipwa? Minazani tujifunze kunyamaza sazingine kama hamna ulazima wakuongea mnaweza kuhisi mmnajenga kumbe mnaharibu kabisaaa… Embu Tufanye Kazi zinazo tuhusu Jamaniii… Nigeria wenzetu sasa wako Hollywood wanaigiza huko… Sisi ata nigeria kwenyewe bado hatuja pasua… Lakin hapa Tupo busy kushabikia ujinga na vitu vya kipumbafu na visivyo na Msaada kwajamiii… Kwastaili hiii… Hollywood tutaiskia na kuiona kwenye TV.no”Ameandika Irene Uwoya.

Irene Uwoya nae ni moja kati ya makada wa CCM waliohusika kwenye kampeni za Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hususani kwenye Kampeni za Rais Magufuli.

 

Comments

comments

You may also like ...