Header

Jay-Z akerwa na Ma’DJ wa kizazi kipya

American rapper Jay-Z performs at Bercy stadium in Paris, October 17, 2013. REUTERS/Benoit Tessier (FRANCE - Tags: ENTERTAINMENT) - RTX14F8N

Rapa Jay-Z amewajia juu Ma’DJ wa siku hizi ambao wanapiga muziki bila kuzingatia vigezo vya wasikilizaji kiasi kwamba radio nyingi zinakosa wasikilizaji.

Jay-Z Kupitia interview aliyofanya na Frank Ocean kupitia Blonded Radio kwenye Apple Music’s Beats 1 rapa Jay Z ambaye ni mmiliki wa kampuni na TIDAL ameongelea mpangilio wa muziki wa radio miaka ya sasa.

Jay Z amelalamikia Ma-Dj wa radio kwa kuangalia zaidi makampuni ya matangazo yanataka nini na umri wa wasikilizaji wengi bila kujali muziki na sanaa.

Utakuta mtu kama Bob Marley hachezwi sasa sababu wasikilizaji wanaumri kati ya miaka 18-34 na ni watoto wakike weupe, sasa Dj anacheza muziki wao tu wa pop bila kujali kuna wasanii wengine kibao ambao wanahitaji hio nafasi“ Amesema Jay-Z .

Jay Z alimalizia kwa kusema radio,muziki, wanamuziki ni sehemu kubwa ya sanaa na haitakiwi kuwa sehemu ya matangazo tu, lazima tuwe na nidhamu.

Comments

comments

You may also like ...