Header

Kuelekea AFCON U-17: TFF yatangaza ratiba ya maandalizi ya Serengeti Boys

TFF imetangaza ratiba ya maandalizi ya Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kabla ya kuelekea kwenye michuano ya AFCON U-17 nchini Gabon.

Kuelekea michuano hiyo TFF imepanga michezo minne ya kujipima nguvu kati ya Marchi 13 hadi April 12 ambapo Serengeti imeomba mechi za kirafiki na Rwanda,Kenya,Guinea Bissau na Burundi.

Hii ni Program ya kocha mkuu na tayari tumeomba mechi za kirafiki ili timu yetu ipate maandalizi ya kutosha kabla ya kuelekea nchini Gabon kwenye michuano ya AFCON U-17 na michezo yote inatarajiwa kuchezewa hapa hapa nyumbani ila kwenye viwanja tofauti tofauti na kwa kuanza tumeomba mechi kati ya majirani zetu kwanza Kenya,Rwanda,Burundi na kama mambo yataenda sawa tutacheza pia na Guinea-Bissau“Amesema Alfred Lucas,Afisa Habari wa TFF.

Comments

comments

You may also like ...