Header

Lulu Diva ataja wasanii wake watano anaowakubali hapa Bongo

Msanii wa Bongo Fleva Lulu Abbas maarufu kwa jina la ‘Lulu Diva’ amefunguka na kutaja wasanii wake watano wa Bongo ambao anawakubali zaidi na kupenda kazi zao.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Lulu Diva amewataja wasanii hao kuwa ni Vanessa Mdee, Belle 9, Dogo Janja, Madee na Barnaba Classic.

Mbali na hilo Lulu Diva amesema kwa kuwa ameingia kwenye muziki sasa hivi atafanya muziki mpaka siku pumzi zake zitakapokata na kusema mashabiki wakae mkao wa kula kwani atakuwa anashusha kazi kwa ajili yao.

Comments

comments

You may also like ...