Header

Waziri Nape Nnauye awakutanisha Diamond Platnumz na Ali Kiba

Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye amewakutanisha Diamond Platnumz na Ali Kiba kwenye kamati ya Uhamasishaji wa timu ya vijana ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kuelekea michuano ya AFCON-U17.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari leo Mh Nape amesema Wizara yake imeteua kamati ya watu 10 ambao watatumika kuwashawishi na kuhamasisha vijana hao kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Akitaja majina ya watu hao ni Wasanii wawili wakubwa nchini Ali Kiba na Diamond Platnumz huku majina mengine ni ya waandishi wa habari na watangazaji na baadhi ya wajasiriamali.

Serengeti Boys inatarajia kuondoka nchini kuelekea India kuweka kambi kwa mwezi mmoja kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea michuano ya AFCON U-17 inayotarajiwa kutimua vumbi mapema mwezi wa Sita.

Comments

comments

You may also like ...