Header

Christian Bella ataja Wasanii wawili ambao anawasikiliza muda mwingi hakuna hata M’bongo

Msanii wa muziki wa Dance na Bongo Fleva Christian Bella amefunguka na kusema kuwa mara nyingi hata ‘idea’ ya muziki wake zinatoka kwa wasanii wawili Chris Brown kutoka Marekani na Koffi Olomide wa DRC kwani ni wasanii ambao anawasikiliza sana.

Akihojiwa na EATV Christian Bella amesema kuwa anapenda kumsikiliza sana kazi za Chris Brown kwanza ni kutokana na ukweli kwamba anampenda msanii huyo lakini pia kingine ni kutokana na majina yao kufanana.

“Mimi kusema kweli sina ‘Role model’ bali mimi napenda muziki mzuri lakini kwa kizazi chetu ukiangalia kwa nje nampenda sana Chris Brown na nasikiliza sana kazi zake, kwa sababu kwanza tunaendana majina ( CB )  Christian Bella, Chris Brown, yaani na mimi ni Breezy vile vile, yaani jamaa ana flow flani ambazo mimi mwenyewe nikimsikiliza nasikia raha lakini hata njia zake pia na feeling zake naposikiliza huwa zinanipa idea, zinanisaidia idea za kuimba lakini huwezi kuelewa kwamba kuna flow flani kwenye kazi zangu kupitia kumsikiliza Chris Brown ndiyo niliweza kuzipata” alisema Christian Bella

Mbali na hapo Christian Bella amesema kwa wasanii wa bendi, msanii anayemkubali na kusikiliza sana kazi zake ni Koffi Olomide, kwani anadai msanii huyo amefanya mambo makubwa sana kwenye muziki wa dansi nchini DRC

Comments

comments

You may also like ...