Header

Lady Jay Dee ataja Wasanii aliowaalika kwenye Uzinduzi wa Album yake mpya ‘Woman’

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Lady Jay Dee anatarajia kuachia Album yake mpya ‘Woman’ mwezi huu Tarehe 31 na tayari kataja baadhi ya majina ya Wasanii ambao watakuwepo kwenye uzinduzi wa Album hiyo  kuwa ni Vanessa Mdee na Ruby ingawaje bado orodha ataendelea kuitaja kadri siku zinavyoenda.

Lady Jay Dee amesema amepanga kuwaalika wasanii wa kike tu kwenye uzinduzi wa Album hiyo kwani anataka kuona wasanii wa kike wakiungana na kusapotiana kwa kila Jambo.

Ni uzinduzi ambao nitapiga karibu nyimbo zangu zote hit kuanzia albamu ya kwanza, kwa hiyo utaona ninahitaji muda mwingi zaidi,Nimewaalika hao kwanza wawili (Vee Money na Ruby) kama watakuwa na nafasi ili nao waimbe pamoja nami, sifikirii sana kualika wasanii wanaume, lakini wakipatikana poa tu, nitashukuru,” Amesema Lady Jay Dee.

 

Comments

comments

You may also like ...