Header

Ushilawadu: Madee amchana live Soudy Brown

Hakuna mtu asiyemjua rais wa Shilawadu kwa sasa hapa Bongo mwenyewe anajiita Soudy Brown kwani hapitwi na kitu mitandaoni lazima akivalie njuga hata ikiwa habari haimhusu yaani lazima aikuze kama sio kutoa maoni.

Sasa leo kupitia mtandao wa Instagram msanii kutoka Tip Top Connection  Tunda Man,aliposti picha ya zamani akiwa na Dogo Janja kama TBT yake na kuandika “Tbt…Still ni mdogo wangu najua upo kwenye mikono salama @dogojanjatz” ndipo Soudy Brown alipokuja kuharibu hali ya hewa Kwa Komenti yake iliyosomeka “Mdogo wako Cku amekua yupo na uwoya

Baada ya Komenti hiyo ndipo Rais wa Manzese ambae pia ni Member wa kundi la Tip Top Connection akaamua kumtolea uvuvi kwa Komenti ya Mauzi iliyosomeka kwa kuhoji  “Hivi Soudy Brown unaolewa lini?” swali ambalo Rais wa Shilawadu hakulijibu kabisa mbali na mashabiki wa Tunda man kumsaidia kujibu.

Comments

comments

You may also like ...