Header

Ali Kiba Aahidi kutoa zawadi hii nono kwa Mashabiki wake

Mfalme wa Bongo Fleva King Kiba maarufu kama Ali Kiba baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini ambako alikuwa  na ziara yake ya Kimuziki pamoja na kukabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA amewaahidi mashabiki wake kuachia Album mwaka huu kama zawadi kwao kutokana na sapoti wanayompatia.

Akizungumza na DizzimOnline Ali Kiba alianza kwa kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo walioonesha kwake kwa kumsubiria muda mrefu bila ya kukata tamaa na kusema endapo mambo yakienda vizuri na yaye anatarajia kuachia albam ambayo atafanya na Wasanii wa kimataifa bila ya kuwasahau hapa bongo.

“Ninachokiona kutoka kwa mashabiki wangu ni upendo mkubwa sana nawambia waendelee kunisapoti kwani nawaandalia zawadi ya Album ambayo itakuwa na vichwa ‘international’ na ‘local’ itakuwa ‘full’ nadhani itatoka mwaka huu kama mambo yakiwa fresh Inshaallah Mungu asaidie”. Alisema Ali Kiba.

Ali Kiba baada ya kumaliza Tour yake Afrika Kusini kwa sasa yupo njiani kuelekea Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki.

Comments

comments

You may also like ...