Header

Mdogo wake na Vanessa Mdee ‘Mimi Mars’ ataja sifa za Mwanaume wa kumuoa

Msanii wa kike anaechipukia kwenye game Marianne Mdee maarufu kama  ‘Mimi Mars’ ambaye ni mdogo wake na Vanessa Mdee amefunguka na kutaja sifa za mwanaume ambaye anahitaji kuwa naye kwenye mahusiano au kuwa mume wake kabisa.

Kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio’Mimi Mars’ amesema yeye hapendi kuwa kwenye mahusiano na mtu maarufu kama ilivyokwa dada yake na kudai yeye anahitaji mwanaume mpole, ambaye hatakuwa kwenye muziki au sekta yoyote ambayo itamfanya kuwa maarufu.

“Mimi siwezi kutoka na mtu maarufu na namuomba Mungu hilo jambo apishie mbali kabisa, kwani mimi napenda nikiwa na mwanaume au mume nikirudi nyumbani nimkute, awe mpole mpole ila asiwe kwenye mambo haya ya muziki, awe mfanyakazi tu ambaye labda anatoka nyumbani asubuhi na kurudi nyumbani mapema ila asiwe mtu maarufu”. Alisema Mimi Mars

Mbali na hilo msanii huyo amesema kuwa mwezi wa nne anaweza kuachia wimbo wake mwingine baada ya kupokelewa vyema na ngoma yake ya ‘Sugar’ kwani anadai mashabiki wamekuwa wakimshauri kuwa asikawie kutoa wimbo mwingine.

Comments

comments

You may also like ...