Header

Wema Sepetu amkaribisha Godbless Lema uraiani kwa ujumbe mzito wenye utata

Baada ya kupata dhamana Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kesi ambayo imedumu kwa muda mrefu kada mpya wa CHADEMA na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu amemtumia ujumbe wa kumfariji uliozua maswali kibao wa kumkaribisha uraiani ili kuendeleza harakati zake.

Wema Sepetu kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika “Karibu Uraiani Mheshimiwa… ✌?✌?” kwenye mtandao wake wa Twitter huku kwenye Instagram akiandika “Nothing In This Thing Called Life Lasts Forever…. Karibu Uraiani Hon. Godbless Lema…Hakuna Kitu wala Hali(situation) inayodumu milele… Hakuna Lenye Mwanzo likakosa kuwa na Mwisho.”

Wema Sepetu ameendelea kusema “hukuwa peke yako hata mimi dhamana yangu ilikuwa ngumu kidogo kutoka lakini God is Good.. Karibu Uraini Mheshimiwa,kuhusu njaa tuliulizwa je tunataka tupikiwe…!?labda nijitambulishe tu, Mimi ni Mwanachama mpya wa Chadema… So usishangae….!!! Welcome Baq

Pia tunashukuru kutoka kwako maana kidogo tumpumzishe huyu Kiumbe anaeitwa Bashite..Welcome Baq Mheshimiwa..Bashite aliuteka mji,wenyewe wanasema Bashite ni Kuzungusha, na mpaka sasa hatujajua Bashite haswa ni kitu gani…! Welcome Back Honorable,Nimeamini kwamba Maamuzi magumu huja na Visa vingi sana… All in All God is Great“Ameandika Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Twitter

Wema Sepetu amehamia Chadema mwezi uliopita akitokea CCM.

Comments

comments

You may also like ...