Header

Muziki Mzuri: Ben Pol,Jux na Baraka The Prince watoa somo kwa Wasanii wa Bongo Fleva

Kama ni mfuatiliaji wa Wasanii hawa  watatu tangia tuuanze mwaka huu utagundua kuwa wapo bize na Ratiba za show zao kwa pamoja na hii ilianzia hapa Dar kwa kwenye show waliyoiita Love Melodies and Lights.

Sasa Wikiendi hii walikuwa Pale Dodoma wote watatu na walichokifanya ni zaidi ya Hapa Dar es salaam kwani asikwambie mtu Live Band ina raha yake na hili mimi nalichukulia kama funzo kwa wasanii wa Bongo Fleva ambao tumezoea uwaona waitumia Playback kwenye Show zao.

Watanzania Tumechoka kuona Show za Play Back kwani ni sawa na kuweka CD magetoni na kusikiliza nyimbo hizo Tazama Show ya 333 Experience ilivyonoga na jinsi wasanii walivyotisha na Live Band.

Hapa Jux akiwaburudisha wakazi wa Dodoma.

Ben Pol ametisha sana mpaka Warembo wakatoa Machozi ya furaha

Baraka The Prince ndiyo alifunika Kabisa hii ni noma sana

Comments

comments

You may also like ...