Header

Fid Q adai Namba 8 aliyoshirikishwa na Daz Baba ilihit kama Muziki ya Darassa

Fid Q amedai kuwa wimbo Namba 8 alioshirikishwa na Daz Baba ulihit kwa ukubwa ule ule ambao wimbo wa Darassa Muziki ulifanya. Amedai kuwa wiki moja tu baada ya kutoka, Daz alikuwa wakifanya show Jumatatu hadi Jumatatu kiasi cha kushindwa kwenda kwenye show nyingine.

“Namba 8 ilipotoka let’s say Jumatatu, halafu kuanzia Friday zinaanza sijui Miss Ilala, Miss Upanga, Miss Temeke, Miss Kinondoni, kwahiyo imetoka Jumatatu Namba 8, kila promota mwenye event yake Jumamosi ya masuala ya urembo anabook namba 8. Mimi siku zote huwa naifananisha namba 8 labda kama Muziki ya Darassa hivi sasa ilivyofanya vizuri. Nafiri Namba 8 ilikuwa hivyo pia,” Fid alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Hata hivyo wawili hao walizinguana baada ya Daz Baba kuanza kumkwepa Fid kwenye show na kwenda na mtu mwingine aliyeimba verse zake kwakuwa alitaka achukue fedha zote mwenyewe.

“Ni kitu ambacho kwangu hakikuwa shida sana, sababu tayari nilikuwa na show zangu lakini siku zote huwa nawish kwamba angeuzingatia mchango wangu na kuniacha nami nije katika shows nikusanye zile senti angekuwa ameplay fair sana.”

Comments

comments

You may also like ...