Header

‘Watanzania huwezi kuwazuia kuzungumza’ – Ray Kigosi.

Ukiambiwa utaje mastaa kadhaa wanaofanya vizuri kwenye soko la filamu Tanzania huwezi kuacha kulitaja jina la Vicent Kigosi (Ray) ambaye umaarufu wake umeanza muda mrefu toka kipindi anashiriki tamthilia na marehemu Kanumba.

Wikiend iliyopita Ray alifanikiwa kuzindua filamu yake mpya inayoitwa Gate Keeper,miezi michache iliyopita Ray aliwahi kuingia kwenye headlines ya kuwa haelewani na Johari ambaye ndiye mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo ya Rj Company.

Kwenye mahojiano yake na Dizzim Online amesema>>’Unajua siku zote Watanzania huwezi kuwazuia kuongea,RJ ni brand ya watu wawili maana yake ni Ray na Johari,labda hawajamuona Johari akiigiza kwa muda mrefu tatizo ni moja kwa Watanzania mkicheza na Johari kila siku watasema Aaah Ray bana kila siku anacheza na Johari,ukisema umpumzishe Johari acheze part zake basi watu watasema kampuni inakaribia kufa’.

Unaweza kumtazama Ray akielezea kila kitu kwa kubonyeza play hapo chini.

Comments

comments

You may also like ...