Header

Kunani Kati Ya DR EDDIE Na OTILE BROWN ??

Huwezi kutaja mafanikio ya msanii OTILE BROWN bila kumtaja DR EDDIE ambaye anamiliki Dreamland Music Empire. Hivi karibuni inasemekana kuna vuta nikuvute za hapa na pale kati ya wawili hao. Kuthibitisha kwamba kuna kitu kinachoendelea, OTILE kupitia mahojiano na runinga ya K24 hivi majuzi alifunguka kuwa kuna tofauti moja mbili za kibiashara “Okay Dr.Eddie namheshimu sana, ni mtu ambaye mpaka hapa nilipofika ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wangu, na tumetoana mbali katika hii biashara ya muziki. Kwahiyo inaweza kufika wakati unahisi mambo hayaendi kama yanavyofaa, so unajikuta mnaanza kukwaruzana kwa njia moja au nyingine na katika biashara issue kama hizo zinatokeaga.” Aliendelea, “But I respect him kwa sababu ana mchango mkubwa sana katika muziki wangu. So it’s not a big issue tutaimaliza soon halafu kila kitu kitakuwa sawa. Naomba tu tuzidi kutoa support.” MSETO itamtafuta DR EDDIE ili aweze kutupa mawili matatu kwa upande wake. Kwa sasa tumedhibitisha kwamba Videos za msanii OTILE hazipo YouTube.

Comments

comments

You may also like ...