Header

Kwa ushahidi huu: Tarajia kuona Kolabo ya Nay wa Mitego na AY

Ebwana kama ulikuwa unajiuliza ni lini Mkongwe wa AY atafanya Kolabo na Nay wa Mitego basi nadhani kiu ya kusikia mdundo wao kwa pamoja inakaribia kukata kwani wawili hao wapo Studio kwa sasa.

Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Twitter ametudokeza kuwa yupo mbioni kuachia Muda wetu Remix na kuahidi kuwa itakuwa na Mastaa kibao “Anytime Muda Wetu Remix itakuwa hewani kuna vichwa kadhaa ndani …!Stay tuned #MudaWetuRemix“Ameandika Nay wa Mitego.

Baada ya hapo masaa mawili mbele akapost picha akiwa na Rapa AY ndani ya studio zake za Free Nation na kuandika “Na El Chapo @AyTanzania #FreeNation kunawaka ??? |#MudaWetu”

So kwa ushahidi huu Kolabo ya Nay wa Mitego na AY ipo njiani na huenda tukamsikia kwenye Muda wetu Remix.

Comments

comments

You may also like ...