Header

Nike wamponza Pierre-Emerick Aubameyang

Klabu ya Borussia Dortmund ipo mbioni kuzungumza na Pierre-Emerick Aubameyang kubadilisha muonekano wa nywele ambao ulikuwa na ishara ya kuonesha alama ya Nike ambao ndiyo wadhamini wake binafsi kwenye mchezo dhidi ya Bayer Leverkusen.

Aubameyang kwenye nywele zake alionekana kuwa na alama ya pink ya kampuni ya Nike kwenye ushindi wa mabao 6-2 ambapo mshambuliaji huyo wa Gabon alifunga goli lake la 20 na 21 la msimu huu.

Wadhamini wa Klabu ya Dortmund PUMA ndiyo wazalishaji wa jezi za klabu hiyo,ambapo mkurugenzi wa kiufundi wa Michael Zorc ameweka wazi kuwa hawataki hilo litokee tena.

Hii pengine imetokana na udhamini wake binafsi wa Nike, kama nitakuwa nimeelewa vyema,” Zorc aliiambia  Sky. “Hii tunaamini haitojirudia baada ya kujadili nae tukishaketi.”Amesema Michael Zorc.

Uongozi wa Klabu yaDortmund bado hawajampa adhabu au kupiga faini Aubameyang baada ya tukio hili na hawajaweka wazi kama watafanya maamuzi yoyote dhidi yake.

 

Comments

comments

You may also like ...