Header

BreakingNews: Zlatan Ibrahimovic afungiwa michezo mitatu

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amefungiwa michezo mitatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko Tyrone Mings mchezaji wa Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu Uingereza.

Adhabu hiyo iliyotolewa na Chama cha mpira nchini Uingereza FA imekuja baada ya kujilidhisha kuwa Kadabra alimpiga kiwiko mchezaji huyo kwa kukusudia.

Hata hivyo FA bado inaendelea na uchunguzi kwa Mings kwani picha za awali zinaonesha alimkanyaga Ibra kichwani kabla ya kufanyia madhambi hayo ya kupigwa kiwiko.

Zlatan atakosa mchezo wa FA dhidi ya Chelsea na michezo miwili ya ligi kuu kati ya Middlesbrough na Westbrom.

Comments

comments

You may also like ...