Header

Man Fongo atumwa na BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemshauri msanii wa singeli Manfongo, kutumia lugha za misamiati na mafumbo katika kazi zake ili kuepusha maneno ya mtaani ambayo yanatafsirika tofauti kwa kuwa muziki huo unasikilizwa na watu wa rika tofauti.

Akizungumza na kituo cha East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo Man Fongo amesema aliitwa na Baraza hilo kushauriwa kutumia lugha nzuri kwenye nyimbo zake ili kuubadilisha muziki huo ambao unaonekana kama muziki wa kihuni.

“Katika wasanii wote wa singeli peke yangu ndiyo nmejiandikisha BASATA, baada ya kutoka India kwenye ‘Show’ wakaniita kwa sababu mimi ndiyo msanii wa singeli mwenye tuzo, wakanambia sasa Manifongo wewe umeshakuwa msanii mkubwa tafadhali kwenye hizi nyimbo zenu inabidi ukawe balozi wa kuwashauri wenzako mtumie maneno ya kiswahili yenye mafumbo, kiswahili mnachotumia kipo wazi sana kama hainaga ushemeji ndo nini?” Alieleza Man Fongo.

Pia Msanii huyo ameweka wazi kuachana na uongozi wake wa mwanzo ambao umeshindwa kuwekeza kwake ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia kazi yake ya Kibaka aliyoitoa siku zilizopita na kushindwa kufanya vizuri.

 

 

Comments

comments

You may also like ...