Header

TENNIS: Rafael Nadal hoi kwa Sam Querrey

Mcheza Tennis Sam Querrey kutoka Marekani amefanikiwa kushinda taji la ATP 2017 katika michuano iliyofanyika nchini Mexico baada ya kumfunga Rafael Nadal kwenye mchezo wa fainali iliyofanyika usiku wa kuamkia jana.

Sam alifanikiwa kushinda fainali hiyo kwa jumla ya 6-3 7-6 (7-3) dhidi ya mpinzani wake huyo ambaye ni raia wa Hispania,Kwa sasa bingwa huyo anashika nafasi ya 26 katika orodha ya wachezaji bora wa tennis duniani akiwa na jumla ya alama 1480 huku Andy Murray wa Uingereza akiongoza orodha hiyo akiwa na jumla ya alama 12040.

Comments

comments

You may also like ...