Header

Barnaba amwaga chozi hadharani

Leo ni siku ya Wanawake Duniani na kila mmoja ameadhimisha kwa hisia mbalimbali kwa kumkumbuka mwanamke ambae kwake anamchukulia kama shujaa ila kwa Barnaba yeye siku ya leo ametoa chozi kabisaa kwani amemkumbuka mama yake ambae ameaga Dunia miaka mingi iliyopita.

Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kwa hisia kali ujumbe ambao amekiri mwenyewe kuwa wakati anaandika hadi vidole vya mikono yake vilipooza kwa muda kwani amemkumbuka sana marehemu mama yake kitu ambacho kimemfanya mpaka aweke emoji ya kikatuni cha Machozi.

Hapo ndani Ya picha kuna picha 3 nimewaza Sana hata nikikupost utoona labda kwa imani na Kirohoo utaona nikawaza Nipost Kabuli ! Nipost sura yako Tu au wewe na mimi mwisho nimeweka Zote mama Mengine mtamaliza mana hata Vidole avina nguvu kwakwlei ?? ………. one off the big Bestfriend aliyezimaga kama mshumaa kabisa |? Maria-Albert-Aloice Face- from ma mom ?? R.I.P #Happywomen”Ameandika Barnaba kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Comments

comments

You may also like ...