Header

Method Mwanjali kukaa nje ya uwanja mwezi mmoja

Beki wa kati wa Simba Method Mwanjali ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa mwezi wote wa Marchi kutokana na maumivu ya Goti aliyopata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prinsons.

Akizungumza na DizzimOnline Daktari wa Klabu ya Simba Yassin Gambe amesema kuwa mwanjali hatakwenda Dodoma na hata husishwa kwenye Program yoyote ya Timu mwezi huu.

Timu yetu inaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya mechi zetu zilizosalia ingawaje tunataarifa ya kushtusha kidogo kwani mchezaji wetu Mwanjali atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi huu (March) wote“Amesema Gambe.

Wekundu hao wa Msimbazi wanatarajia kwenda mkoani Dodoma kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.

Comments

comments

You may also like ...