Header

Nicki Minaj adai hawezi kujibu uongo wa Remy Ma

Nicki Minaj hana mpango wa kuijibu diss track ya Remy Ma, Shether.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na mtandao wa TMZ, Nicki anahisi kuwa shutuma nyingi ambazo Remy alizisema, zimetajwa kuwa ni za uongo na watu mbalimbali wakiwemo Lil Wayne, Trey Songz, Ebro na Safaree waliotajwa.

Pamoja na mambo mengi kuonekana kula kwa Nicki hususan shutuma za kuwa ametembea na watu kibao, rapper huyo hana mpango wa kujitetea.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa Nicki hajajificha, bali yuko busy na mambo mengi ikiwemo kushoot video za ngoma alizoshirikishwa na Future na Gucci Mane. Pia amezindua app yake mpya.

Nicki anaamini kuwa anashinda bifu hiyo kwa kuamua kubakia kimya.

Comments

comments

You may also like ...