Header

Wema Sepetu amuunga mkono Paul Makonda

Miss Tanzania 2006 Mrembo Wema Sepetu ambae ni Kamanda mpya wa Chama cha CHADEMA ameadhimisha siku ya Wanawake kwa kupanda miti huko mkoani Morogoro na katika kile kinachoonekana ni kulinda mazingira.

Wema Sepetu ametumia mawazo yale yale ya kampeni ya ‘mti wangu’ ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda ambayo ilikuwa na lengo la kulinda mazingira.

Wema Sepetu aliyevaa T-Shirt nyeusi

So huenda Wema Sepetu akatumia ushawishi wake kutangaza kampeni kubwa za kulinda mazingira kwani kwa sasa nchi yetu imekumbwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kwa hilo kila mtanzania atamsapoti Wema Sepetu namshauri pia kampeni hiyo ianzie mkoani Dodoma ambako hali ya ukame imekithiri.

Leo ni siku ya wanawake Duniani, na kama mwanamke nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabili ya Maji… Wote tunajua kuwa mwanamke ndo anaekerwa zaidi katika upatikanaji wa maji… Labda haitotusaidia leo wala kesho, lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu hapo baadae…. Morogoro ni eneo linalosadikika kuwa Chanzo cha Maji hata yale tunayotumia Mkoani kwetu (Daressalaam)… Ninajiskia faraja kuwa kutakuwa na helping hand yangu somewhere when it comes to Water supply in my society… Mazingira yetu hayana Itikadi wala Vyama, Yanagusa kila mtu… I feel honored to be part of this activity… Tumetoka Kata ya Kilakala and now tunaelekea kwenye Chanzo kingine kinachoitwa Mambogo.“Ameandika Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Comments

comments

You may also like ...