Header

‘Kuja na Clothing line yangu ya mavazi sifikirii’ – Belle Nine.

Biashara ya muziki imekua extended sana kiasi kwamba wasanii kwa sasa hawategemei tena shows peke yake au kuuza nyimbo tu,sasa hivi wasanii wamekua wakifanya biashara ya vitu vingi kupitia brand zao.

Miongoni mwa vitu ambavyo vimekua wasanii wengi vikiwaingizia pesa ni kutengeneza clothing line ambapo Kibongobongo tumewaona watu kama Diamond,Shetta,Weusi,Tiptop Connection,Jux,Yamoto Band na baadhi yao wakiingiza pesa kupitia brand hizo.

Belle Nine kupitia XXL ya Clouds FM amesema yeye hafikirii kabisa kuja na clothing line yake>’Kuja na line yangu ya mavazi kiukweli sifikirii lakini watu wengi wamekua wakicomment kunambia hiyo kitu,nadhani nahitaji reseach kujua hiyo biashara ina faida gani na natumia mbinu zipi kutake over’

‘kwenye kila kitu inabidi upiganie namba moja,napenda kuwa namba moja najua thamani ya namba moja siwezi kuleta clothing line bila kuwa na research ya kutosha nijue kabisa naingia kwenye changamoto gani’.

Comments

comments

You may also like ...