Header

Diamond aja na kampuni yake ya kuuza muziki Afrika…

Kwenye hatua za ukuaji wa muziki wa Wanamuziki wenyewe kwa hiki alichokifanya Diamond ni kikubwa zaidi,March 09 2017 anaiandika historia nyingine kwa kutambulisha platfoam mpya itakayokua inashughulika na uuzaji wa kazi za wasanii wa ndani.

Kwenye maelezo yake Diamond amesema>>’kuanzia sasa Wasafi Dot com ndio sehemu rasmi  ya kuweza kujipatia Nyimbo za wasani wako wote pendwa toka hapa nchini Tanzania na nje ya tanzania’

‘Lengo kuu la kuanzisha mtandao huu ni kuweza kuwarahisishia Mashabiki na wadau wa mziki wetu muweze kujipatia kazi za wasani wenu zikiwa zina Quality ama ubora sahihi, na haraka lakini pia kutusapot vijana ama watoto wenu nasi tuweze kuendelea kuwatengenezea kazi zenye ubora zaidi’

‘Sababu nyingine ya kuamua kuanzisha mtandao huu ni jinsi mlivyokuwa mnatusapoti vijana wenu kwa kununua kazi zetu halafU mwisho wa siku baadhi ya wamiliki wa mitandao wakawa hawatupi haki zetu tunayostahili, yaani wakawa wanatudhulumu na kunufaika wao huku sie wasanii wenu tukiishia kuambulia umaarufu wa majina  ila maisha yetu halisi “pangu pakavu”…hii ilituumiza na kutuliza sana, karibu miaka yote’

‘Kwenye mtandao huu wa Wasafi dot com tumeweka njia mbalimbali za kununua nyimbo,kupitia account ya simu ya mitandao yote ya simu Afrika,pia kununua kwa njia ya Card ya Benki mfano: Master Card, Visa card na njia zote za kibenki’

‘Matumaini yetu kuwa  mtatusapoti kwa kununua kazi zetu Wasafi dot com na panapo majaaliwa kwa mara ya kwanza ijumaa ya kesho Harmonize ataachia wimbo wake mpya Uitwao NAMBIE na utakuwa unapatikana Wasafi dot com’

‘Nitasikitika sana sana nikiona ama kusikia shabiki yetu anakuwa mtu wa kwanza kuomba kutumiwa  nyimbo badala ya kuingia Wasafi dot com kudownload hapo… kesho  hiyohiyo pia kutakuwa na nyimbo za wasanii wengine zaidi uwapendao…. @Wasafidotcom #WhereTheHitsBelong’ – Diamond Platnumz.

Uliisikia hii ya Barakah Da Prince kurudiana na Naj?iko hapa pia,Bonyeza play kutazama.

Comments

comments

You may also like ...