Header

Nicki Minaj hana cha kupoteza kwa Remy Ma

Wakati watu wengi na mashabiki wa muziki wa Hip Hop Duniani wakisubiri jibu la Nicki Minaj kwa rapa mwenzie Remy Ma baada ya kumdiss kwenye ngoma yake ya ‘shETHER’ basi toa mawazo hayo kwani rapa huyo hana cha kupoteza.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Menejimenti yake ya Young Money imethibitisha taarifa hizo kuwa Nicki Minaj hana mpango wa kumjibu Remy Ma badala yake hata kitendo cha kunyamaza ni jibu tosha kwa Rapa huyo.

Young Money imesema Nicki Minaj hayuko mafichoni, anafanya video za Kolabo na wasanii wengine kama Future na Gucci Mane na alikuwepo kwenye maonyesha ya mavazi ya Paris Wikiendi iliyopita akiwa na furaha tele.

Comments

comments

You may also like ...