Header

Pambano la Manny Pacquiao na Amir Khan laota mbawa

Pambano kati ya Bondia Amir Khan na Manny Pacquiao lililotarajiwa kufanyika mwezi ujao kulingana na promota Bob Arum limeota mbawa.

Mabondia hao wawili walikuwa wametangaza pambano hilo kufanyika mnamo mwezi Aprili 28 katika mtandao wa Twitter mwisho wa mwezi Februari huku UAE ikitajwa kuwa eneo la pigano hilo.

Lakini Promota wa pambano hilo Arum amekiambia kituo cha runinga cha ESPN kuwa Pambano hilo limefutiliwa mbali,”Ninazungumzia kuhusu pendekezo jingine lakini sio Khan. Khan hatakuwa tena mpinzani wa Manny”Amesema Promota huyo.

Pambano hilo la mwezi Aprili lilipangwa baada ya mashabiki wa Paqcuiao katika mtandao wa Twitter kumpigia  Khan kuwa mpinzani ambaye wangependelea bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 kupigana naye.

Khan ambaye mwenye umri wa miaka 30 aliyeshinda medali ya fedha katika uzani wa Lightweight katika michezo ya Olimpiki ya 2004, alimshinda Kell Brook, raia wa Australia Jeff Horn na Mmarekani Terence Crawford kwa asilimia 48 ya kura hizo zilizofanywa na Pacquiao.

                                                                  CHANZO:MTANDAO WA BBC

Comments

comments

You may also like ...