Header

Wakazi amkumbuka The Notorious B.I.G

Leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Rapa Notorious B.I.G ambae alifariki tarehe kama ya leo March 09-1997 kwa kupigwa risasi huko jijini Los Angeles nchini Marekani,kifo ambacho hakitasahaulika kirahisi kwenye kichwa cha Rapa kutoka Tanzania Wakazi.

Wakazi amekuwa msanii wa kwanza leo kutweet kwenye mitandao ya kijamii hapa Bongo kumkumbuka Rapa huyo kwa kuandika “Cause the greatest rapper of all time died on March 9th…. Rest In Peace BIG, it’s because of you now at least I know what beef is

Kwa maelezo machache Wakazi amejifunza vitu vingi sana kutoka kwa Rapa huyo ambae anatajwa kama rapa bora kwa muda wote ikiwemo neno ‘Beef’ na jinsi ya utungaji wa mashairi kuendana na Nyakati.

Naikumbuka sana siku hii kwani ni siku ambayo ulimwengu ulimpoteza rapa mkubwa sana BIG amewa’Inspire watu wengi sana ikiwemo na mimi kwani utungaji wake wa mashairi ulikuwa unadumu mpaka leo hii nikisikiliza nyimbo zake bado kuna vitu najifunza kwenye uandishi wangu jamaa alikuwa Real sana“Amesema Wakazi wakati akiongea na DizzimOnline.

Wakazi aliendelea kusema “BIG amenifanya nijue tofauti ya Beef na Battle” akifafanua utofauti wa Beef na Battle amesema beef ni kufa au kupona yaani ukisikia beef ni lazima watu wajilinde hata kwa silaha za moto kwani unaweza ukapoteza hata maisha ya familia yako hivyo hata hizi tunazozisikia sio beef ni Battle tuu.

Comments

comments

You may also like ...