Header

Bill Nass – ‘Video ya Mazoea imenipeleka mbali sana’

Rapa kutoka Tanzania Billnass amekiri wazi kuwa video yake mpya ya wimbo wa Mazoea imempeleka mbali sana kwani imesambaa karibia kila sehemu barani Afrika.

Billnass amesema kwa sasa wimbo huo licha ya kufanya vizuri hapa Bongo pia hata nje ya Tanzania kwenye media za kimataifa wimbo huo umeingia kwenye Top Ten .

Video ya Mazoezi imenifungulia milango mingi sana kwani tangia nimeiachia mpaka leo video imekwenda kwa kasi ya ajabu,na imekuwa tofauti na nyimbo zangu za awali kwani imepenya mpaka kwenye top ten za Trace Urban,Sound City na MTV Base so hii imenipa faraja sana“Amesema Billnass kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Wiki iliyopita Billnass aliahidi kuachia ngoma mpya endapo tu video yake mpya ya mazoea ifikishe Views Milioni moja na mpaka sasa video hiyo ina views 751,330 kwenye mtandao wa Yotube.

JE,ULIPITWA NA HII YA BILLNASS KUZUNGUMZIA MUZIKI WA HIP HOP JINSI UNAVYOKUA??BONYEZA PLAY HAPA CHINI

 

Comments

comments

You may also like ...