Header

lady Jay Dee na mpenzi wake ‘Spicy’ wamwagana??

Mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na stori kubwa sana kumuhusu msanii wa kike Lady Jay Dee kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kutoka Nigeria aliejulikana kwa jina la ‘Spicy’ ambae ni raia wa Nigeria.

Sasa leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ameandika ujumbe ambao umeleta maswali kibao kwa mashabiki wake na ujumbe huo ulisomeka”Ni kweli niliamua kuondoka, nikidhani nitapendwa niendako?HAKUNA? Nilidhani nitakuta tofauti yoyote mpaka sasa sijaona“.

Lady Jay Dee anaetarajia kuachia Album yake mpya ya ya ‘Woman’ mwishoni mwa mwezi huu hajatoa ufafanuzi wowote kuzungumzia kusudi la ujumbe huo.Baki na sisi tutakujuza kila litakalojiri kwani hatupitwi na habari yoyote ile ya burudani.

Comments

comments

You may also like ...