Header

Majani akitaja kinachomkwamisha Cpwaa kimuziki

Hivi karibuni Cpwaa alionekana studio akirekodi wimbo kwenye studio za Bongo Records na producer Majani. Alisema kuwa huo utakuwa ujio wake mpya na mzito baada ya kukaa kimya kwa muda.

Hata hivyo mambo yanaweza yasiwe na uharaka kama alivyoashiria, kwa mujibu wa Majani. Akizungumza kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Majani alisema Cpwaa ana matatizo ya kukurupuka.

“Cpwaa anakurupukaa, hana msimamo,” alisema. Alidai kuwa baada tu ya kurekodi wimbo huo alitaka wautoe wakati Majani alitaka warekodi nyimbo zingine zaidi kabla ya kutoka tena.

“Cpwaa is a monster, asiridhike na tulichokuwa nacho, he needs to get back to the studio, get you momentum back,” aliongeza.

Comments

comments

You may also like ...