Header

Huyu ndiyo staa mwingine kutoka Nigeria aliyepata shavu kwenye Album mpya ya Swizz Beatz ‘Zone’

Producer na Rapa maarufu kutoka Marekani Swizz Beatz anaendelea kutoa mashavu kwa wasanii kutoka Afrika tena kwa njia tofauti tofauti na mara hii amemuongeza msanii mwingine kutoka Nigeria kwenye Album yake mpya iitwayo ‘Zone’.

Image result for mc galaxy and swizz beatz

Alicia Keys,Swizz Beatz na MC Galaxy

Swizz Beatz amemchagua msanii kutoka Nigeria ajulikanae kwa jina la MC Galaxy aliyewahi kutamba na hits kama Sekem kuwa nae ni moja ya wasanii watakaokuwemo kwenye album yake mpya.

Mchekeshaji huyu aliyegeuka muimbaji atasikika kwenye album mpya ya Swizz Beatz iliyopewa jina ‘Zone’,SwizzBeats na Alicia Keys walipost kwenye snapchat clip ya wimbo huo na kusikika sauti ya Mc Galaxy akiimba kwa lugha ya kwao ya lbibio.

Wimbo wa MC Galaxy “Sekem” ulitumika kwenye filamu ya Hollywood ‘Queen of Katwe‘ nakufanyiwa remix na Swizz Beatz,na kwenye Album hiyo atakuwepo pia Wizkid.

Comments

comments

You may also like ...