Header

‘Siko tayari kwenda kusajiliwa label ya msanii yoyote wa Tanzania’ – Matonya.

Ukubwa wa majina ya wasanii wa Tanzania unapelekea sasa hivi baadhi yao kuamua kutengeneza label zao kwa ajili ya kuwasimamia wasanii wenzao ambao kwa namna moja au nyingine inaaminika ikitumika nguvu moja inaweza kusaidia kusukuma zaidi muziki huu kufika mbali zaidi.

Barnaba,Navykenzo,Vanessa Mdee,Diamond Platnumz,Nay wa mitego ni baadhi ya wasanii walioamua kukaa na kutengeneza label zao ili kusaidia wasanii wengine kutoka na kutimiza ndoto zao zaidi,Hit maker wa singo kadhaa ikiwemo ‘Vaileti’ Matonya amesema hayuko tayari kusainiwa na label yoyote kati ya hizi zinazomilikiwa na wasanii hao.

Kwenye mahojiano yake na XXL ya Clouds FM Matonya amesema>>’Kuwa chini ya Label siko tayari lakini kwenda kuongeza nguvu ya kazi kusema tunaweka akili zetu sehemu moja kwa ajili ya kufanya kazi kwa pamoja kushirikiana kuweka mawazo kwa sababu tunaamini kwamba katika hizo label zote zinafanya vizuri’

‘Mimi sasa hivi siko tayari kwenda kufanya kazi sijui kusajiliwa label siko tayari,labda kuweka akili zetu sehemu moja kuhakikisha kila kitu tunakiweka sawa niko tayari kwa sababu sisi sote tunapigania njia moja ni kuweka nguvu kwa ajili ya kusogeza muziki wetu’. – Matonya.

Comments

comments

You may also like ...