Header

‘Ni kweli Yamoto Band tumewatoa kambini na walitakiwa kutoka’ – Mh.Temba.

Yamoto Band wameingia kwenye headlines mara kadhaa za kusemekana kuwa hawana maelewano mazuri na uongozi wa kundi hilo ambalo linaongozwa na Said Fela (Diwani wa Kilungule) na taarifa hizi zimekuja baada ya taarifa ya kuwa hata pale kambini wanapoishi wasanii hao wamehama na kila mmoja kaenda kuishi peke yake.

Mmoja kati ya viongozi wa kundi hilo Mheshimiwa Temba kupitia XXL ya Clouds FM amesema>>’Kutoka kambini ni kweli na sio walitoka lakini walitakiwa kutoka kwa sababu walishakua wakubwa tayari wale,washakua na familia washakua na watoto inabidi waende wakapange sehemu nyingine’

‘Zile nyumba zao tulizokuwa tumezijenga bado hazijamilika na kule ni ngumu kwenda kwa sababu kuna vitu havijawa sawa kama maji bado hayajafika,ikabidi tuwaaambie wakapange sehemu nyingine,kwa uelewa mdogo wa watu wakaanza kusema Ooh mbona wameondoka kwenye kile kituo’

‘Tunahitaji kuweka wengine waweze kukua kama wale madada 6 kuna yule dansa Chiba,ukizungumza pesa mbona zipo,pesa kila mtu alikua anapata pesa zake zingine zinaenda kwenye nyumba,kungekua na matatizo walitakiwa waje wenyewe wazungumza au uongozi tuzungumze’. – Mh. Temba.

Kama wewe ni shabiki wa Darassa,Samatta,Fid Q na Nicki Minaj Cheki stori zao kubwa hapa kwa kubonyeza play hapa chini.

 

Comments

comments

You may also like ...