Header

Baada ya Ben Pol kuvutiwa na Lebo ya Cheusi Dawa: Hatimae Fid Q amjibu

Baada ya msanii wa Bongo Fleva Ben pol mwezi uliopita kukiri wazi kuwa endapo Fid Q ataanzisha lebo ya muziki basi yupo tayari kusaini nae kwenye hiyo lebo sasa tayari lebo hiyo Fid Q ameshaifungua ‘Cheusi Dawa’ na kusaini msanii mmoja mpaka sasa ambae ni Big Jahman na kwa kuongezea Fid Q amemjibu mkali huyo wa RnB .

‘FID Q AKIANZISHA LABEL NAWEZA KUFANYA NAE KAZI’ – BEN POL.

Fid Q amemjibu Ben Pol kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm na kusema kuwa yupo tayari kufanya nae kazi kwani ni moja ya wasanii wenye vipaji vya hali ya juu na hata yeye anamkubali sana na huwa anafuatilia sana nyimbo zake .

Fid Q Aliendelea kumzungumzia Ben Pol kwa kusema anamheshimu tangia zamani na hata wimbo wake wa Moyo mashine ulivyotoka alipata bahati ya kusikilizishwa na akatoa Go ahead ya wimbo huo kutoka kwani aliona ni wimbo mkali sana.

 

Comments

comments

You may also like ...