Header

Bosi wa label ya Chocolate City Audu Maikori atoka nje kwa dhamana

Bosi wa label ya Chocolate City, Audu Maikori, ameachiwa kwa dhamana baada ya kupandiswa kizimbani kwenye mahakama ya Kaduna nchini Nigeria. Wakili wa Maikori, John Danfulani, amesema mteja wake alipewa dhamana Jumatatu mchana.

Maikori anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi wa fujo yaliyofunguliwa na serikali ya jimbo la Kaduna kufuatia tweets zake zilizodai kufanyika mauaji ya wanafunzi kusini mwa Kaduna.

Alikamatwa Ijumaa iliyopita na kushikiliwa na polisi. Wakili wake amesema bosi huyo amepewa dhamana baada ya kusomewa shtaka lake kuhusiana na sheria tata ya makosa ya mtandao.

Kesi yake itasikilizwa tena May 24.

Comments

comments

You may also like ...