Header

#EUFAChampionsLeague: Leicester City kutupa karata yao ya mwisho dhidi ya Sevilla,leo usiku

Mabingwa wa tetezi wa Ligi kuu England Leicester City leo wataamua kusuka au kunyoa katika michuano ya Kombe la Mabingwa Ulaya, itakaposhuka dimbani kurudiana na Sevilla, ikiwa chini ya kocha mpya,Craig Shakespeare.

Msaidizi huyo wa zamani wa kocha aliyetimuliwa Claudio Ranieri, alitangazwa kuwa kocha Leicstere City hadi mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa Uingereza kushinda mechi mbili dhidi ya Liverpool na Hull City katika EPL na kufufua matumaini ya kutoshuka daraja.

Leo kocha huyo, atawaongoza Mbweha hao kwa mara ya kwanza kama kocha Mkuu ili kupindua matokeo ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Sevilla, wiki mbili zilizopita,Mchezo mwingine wa pili hii leo, ni pale  mabingwa wa Italia Juventus, walioshinda mechi ya Kwanza 2-0 Ugenini, wapo kwao Juventus Stadium Jijini Turin, Italia kurudiana na FC Porto.

Comments

comments

You may also like ...