Header

Jay-Z aongeza kichwa kingine kwenye lebo yake ya ‘Roc Nation Latin’

Lebo ya Roc Nation Latin inayomilikiwa na Rapa Jay-Z imeongeza msanii mwingine wa kike hii yote Ili kuweza kuboresha utendaji kazi wake na kupanua mipaka ya himaya yake huku nguvu kubwa ya kumpata msanii huyo mpya imepigwa tafu na Msanii Romeo Santos.

                                                                                  Farina

Msanii huyo aliyesainiwa ni Rapa Farina kutoka Colombia na rapa huyo amepata bahati hiyo baada ya CEO wa Roc Nation Latin ambae pia ni msanii Romeo Santos kugundua ukali wake kwa kupitia nyimbo zake.

Akizungumza na Mtandao wa Billboard.com/Latin Romeo amesema alisikia nyimbo tatu tu za Farina nakugundua kuwa anafaa kusajiliwa Roc Nation Latin. Farina tayari anafanya kazi na Wyclef Jean kutengeneza album yake mpya ya Mejor que yo.

Roc Nation Latin hili ni tawi la lebo ya Roc Nation ambalo linadili na Wasanii kutoka kanda ya Amerika ya Kusini na lipo chini ya Jay-Z  na kwasasa kuna Wasanii wanne waliosainiwa na Lebo hiyo ambao ni Mozart La Para, Jayro Rosado, Karen Rodriguez, Victoria “La Mala” na Mr. Paradise.

Comments

comments

You may also like ...