Header

Jaguar akanusha taarifa za kushikiliwa na Polisi Kenya kwa tuhuma za mauaji.

Miongoni mwa taarifa zilizotoka leo March 14 na kuandikwa kwenye magazeti ya Tanzania na Kenya ni pamoja na hii ya Jaguar kusemekana kuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kenya kwa tuhuma za mauaji yaliyotokea Kenya sehemu ambako alikuwepo kwenye mkutano wa hadhara.

Kupitia XXL ya Clouds FM Jaguar amesema >>’Hizo sio tuhuma za kweli kwa sababu kuna watu wanaeneza propaganda,Unajua nawania kiti cha Ubunge cha Starehe katika kaunti ya Nairobi sasa kuna kijana nasikia walipigana mmoja akafariki,ukiangalia taarifa iliyoandikwa na familia yake inasema kuwa alifariki saa moja na nusu usiku na mimi niliondoka saa kumi na moja na nusu jioni sehemu inaitwa Ziwani’

‘Kijana mwenyewe hakufia ziwani mahali nilikuwa nasikia alipatikana Kariakoo,lakini hakuna polisi alinipigia simu nimesoma magazeti ya Kenya wameandikwa nitaitwa lakini hakuna mtu aliyeniita,nilishirikiana na familia yake kulipia baadhi ya huduma na kuhakikisha anapelekwa kwao kisumu’

‘Nilienda mtaani kule kusaidia kuwapa mashine za kuoshea magari kwa vijana nikamaliza nikatoka kabla ya tukio hilo kutokea’. -Jaguar.

Kwa maneno haya ni dhahiri hili dongo alilolitoa Manfongo linaenda kwa Sholomwamba,bonyeza play kutazama.

Comments

comments

You may also like ...