Header

TFF yatangaza mchezaji bora wa mwezi Februari VPL msimu wa 2016/2017

Shirikisho la chama cha mpira nchini TFF limemtangaza mchezaji bora wa Mwezi wa Februari kama ilivyokuwa desturi yao ya kuchagua mchezaji aliyefanya vizuri zaidi kwenye mwezi husika.

Mchezaji wa timu ya Mwadui FC, Hassan Kabunda ndiye aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Februari kwa msimu wa 2016/2017.

Hassan Kabunda

 

Kabunda aliwashinda wachezaji Laudit Mavugo wa Simba SC na Ibrahim Ajib pia wa Simba SC.

Katika mechi tatu ambazo Mwadui ilicheza kwa mwezi huo, Kabunda alicheza kwa dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya pointi sita zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika Msimamo wa Ligi kwa mwezi huo wa Februari (kutoka nafasi ya nane hadi ya sita).

Kabunda alifunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo tatu kati ya sita iliyofunga timu yake. Kiungo huyo mshambuliaji alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi.

Kwa kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF)

Comments

comments

You may also like ...