Header

Vita ya Kodi: TRA yaikaba koo TFF

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ imezifungia ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo na kuamrisha kuacha kila kitu ndani.

 

Kampuni ya Yono Auction Mart ‘YAM’ walihusika katika kuzifunga ofisi hizo na kuwataka wafanyakazi wote kutoka nje ya ofisi na kuacha kilakitu ndani,Uamuzi ambao umeigharimu timu ya vijana Taifa ya vijana Serengeti Boys ambao walikuwa wanatumia uwanja wa Karume kwa mazoezi ya maandalizi ya AFCON U-17.

Awali TFF walikuwa wanadaiwa na TRA na kuzuia baadhi ya magari yakiwemo yanayotumiwa na timu za taifa ambzo baadae yaliachiliwa na kuanza kutumika tena.

Comments

comments

You may also like ...