Header

Jose Mourinho amkingia kifua Pogba.

Kocha mkuu wa Klabu ya Manchester United mreno José Mourinho amewajia juu wale wote waomsema vibaya Paul Pogba na kusema kuwa kiungo huyo wanamuonea wivu kwa fedha zake.

Mourinho na Pogba

United ilimnunua Pogba kwa pauni million 94 na wachambuzi wengi wanakosoa kuwa Pogba haoneshi kiwango cha dhamani ya kiasi cha pesa alichonunuliwa uwanjani.

“Sio kosa la Paul yeye anapata mara kumi ya fedha walizokuwa napata wachezaj wazuri kipindi cha nyuma. sio kosa lake kama baadhi ya wachambuzi wako kwenye matatizo ya maisha yao wanahitaji kupigana na maisha wakati huo Paul ni millinea mkubwa sio kosa lake…” Alisema José Mourinho

Leo Manchester United wanaikaribisha Rostov Fc kwenye dimba la Old Trafford ukiwa ni mchezo wa marudiano wa Europa Ligi.

Comments

comments

You may also like ...