Header

“Nabadilika kwa lengo la kufika Hollywood” – Idris Sultan.

Mshindi wa Big Brother Hotshots,muigizaji na mchekeshaji ‘Idris Sultan’ ni mmoja ya mastaa  wa bongo waliopata nafasi ya kushiriki katika movie mpya iliyozinduliwa tarehe 15/03 mwaka huu inayokwenda kwa jina la KIUMENI.

Filamu ya KIUMENI ambayo imeandikwa na Daniel Manege na Ernest Napoleon ni moja ya filamu inayoonekana wazi kuleta mabadiliko makubwa sana katika tasnia ya filamu Tanzania ikiwa imeandaliwa nchini Tanzania na baadhi ya mambo kumaliziwa nchini Marekani.

Akizungumziana na Dizzim Online Idris amesema nia yake ya kuendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania ni kufika HollyWood hivyo kubadilika kwake anaamini ni msingi kubwa yeye kufanikisha hilo kwakuwa maoni ya waliopata kuitazama filamu hiyo ambayo kwake ni filamu ya kwanza wameonesha kupendezwa na uwezo wake.

Akielezea nafasi aliyoicheza katika filamu ya KIUMENI  ”…ni character ambayo nimejaribu kuwaonyesha watu kuwa naweza kufanya vitu tofauti tofauti na nina lengo kubwa sana la kwenda Hollywood,kwa hiyo siweza kubaki kawenye character moja…” Amesema Idris.

Hata hivyo mbali na Idris kushiriki wapo wengine Bongo Movie stars ambao ni pamoja na Antu Mandoza,Irene Paul Akbar Thabeet na wengine wa ziada.

 

 

Comments

comments

You may also like ...