Header

‘Najua watu wana hamu ya kumuona mwanangu,ukifika muda watamuona’ -Ray Kigosi.

Vincent Kigosi aka Ray ni miongoni mwa wazazi wapya kwa mwaka 2017 baada ya kuufungua kwa kupata mtoto wake wa kwanza na baby mama wake Chuchu Hans na mtoto huyo amepewa jina la Jaden.

Toka taarifa ya mwanzo inatoka juu ya mtoto huyo,Ray hajawahi kupost picha inayomuonyesha mtoto huyo akiwa full zaidi ya nusu nusu kama ilivyotokea kwa mastaa kadhaa kama Jay Z wakati anazaliwa mtoto wake wa kwanza na Diamond kwa upande wa watoto wake wote wawili.

Mic ya DizzimOnline ilimfikia kutaka kufahamu kama hii mipango ni kama walivyofanya mastaa wengine na lini atakua tayari kumuonyesha mtoto wao>>’Watu wana hamu sana ya kumuona lakini ukifika muda wake watamuona wasiwe na wasiwasi wowote’

‘Nampenda sana mwanangu sababu ndiye mtoto wangu wa kwanza,mpango upo na bahati nzuri muda haujafika tu ukifika nitamuonyesha,siwezi kukaa miaka yote nisimuonyeshe hapana lakini bado mdogo sana unajua macho ya watu tena,namuacha akue kidogo nitamuonyesha’. – Ray Kigosi.

Comments

comments

You may also like ...