Header

Tarajia kumuona Joh Makini kwenye movie

Joh Makini na Muigizaji Antu Mandoza kwenye uzinduzi wa filamu ya KIUMENI.

Rapa Joh Makini anayefanya poa na kazi yake ya WAYA amewataka mashabiki wa muziki na filamu watarajie kumuona kwenye kiwanda cha filamu.

Akizungumza na Dizzim Online Joh ameitaja safari yake kimaisha kutoka Sinoni Daraja mbili,Arusha mpaka kufika alipofika ni movie tosha kama rapa.

“…mimi naamini maisha yangu yenyewe is like a movie ni kiasi cha kuamua tu kuyaweza mbele ya camera kufanya kitu…na naamini mungu amenipa vitu kwa hiyo siku moja usishangae siku moja ukiniona pia kama nimeamua kucheza movie… is just amatter of time…” alisema Joh Makini.

Hata hivyo Joh Makini amewapongeza sana wadau wanozidi kuwekeza katika Filamu Tanzania na kuponeza hatua filamu ilipofikia inaonesha userious.

 

 

Comments

comments

You may also like ...