Header

Yanga kuwakosa wachezaji muhimu 7 kwenye mchezo wao dhidi ya Zanaco FC

Kuelekea mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika klabu ya Yanga itawakosa washambuliaji wake wa kutumainiwa na Mabeki pamoja na Goli kipa mmoja kwenye kikosi cha wachezaji 20 ambao watapambana dhidi ya Zanaco FC.

Taarifa kutoka kwa Katibu mkuu wa Klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa Mrundi Amis Tambwe na Donald Ngoma ni majeruhi mbali na hao pia klabu itawakosa kipa Beno Kakolanya, beki Pato Ngonyani, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji wengine wawili, wote wazawa, Malimi Busungu na Matheo Anthony ambao pia ni wagonjwa.

Akitaja majina ya Wachezaji 20 wanaondoka kuelekea zambia amesema ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’, Oscar Joshua, Mwinyi Haji Mngwali, Hassan Kessy, Juma Abdul, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Wengine ni pamoja na Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Justine Zulu, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emanuel Martin.

Yanga inahitaji ushindi wa ugenini Jumamosi ili kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments

comments

You may also like ...