Header

Zanzibar yapata uanachama wa CAF

Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF limetambua Ombi la Zanzibar kuwa mwanachama Rasmi wa CAF limepitishwa bila kupingwa Yaani Un-animous Approval. Hii inamaanisha kuwa Zanzibar inakuwa mwanachama wa 55 wa CAF.

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Rais wa CAF Issa Hayatou

Zanzibar imepewa uanachama wa kudumu wa CAF leo Alhamis kwenye mkutano wa 39 huko jijini Addis Ababa, Ethiopia,Pendekezo hilo lilipelekwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndugu, Jamal Malinzi na lilipokelewa na wajumbe 54 wengin waliokuwepo.

Hii maana yake ni kuwa kwa sasa CAF ndio shirikisho mwanachama wa FIFA kwa upande wa mabara lenye wanachama wengi zaidi kuliko wote.

Vilabu vya Zanzibar vimekuwa vikishiriki mashindano mbalimbali ya CAF lakini kwa ngazi ya kitaifa hawakuwa na ruhusa na walicheza kwa kuungana na Tanzania bara na kushiriki kama Tanzania.

Kwa maana hiyo basi, chama cha soka cha Zanzibar kitapata uwezeshaji wa kifedha moja kwa moja kutoka CAF na FIFA kwa ajili ya timu ya taifa.

Comments

comments

You may also like ...